Njia tofauti za kupata pointi

Shiriki katika tafiti

Unapomaliza tafiti, utapata pointi ambazo zinaweza kubadilishwa na zawadi mbalimbali. Tutakutumia mwaliko wa utafiti kwa barua pepe na pia waweza kuona mwaliko wako hapa kwenye mtandao wetu. Unaweza kupata pointi baada ya kila utafiti unaojaza. Idadi ya pointi inategemea urefu na utata wa utafiti.
Angalia nini unaweza kuchagua kutoka kwa pointi zako

Alika marafiki

Alika marafiki wajiandikishe kama washiriki wa OpinionArena. Tutakupa pointi 60 kwa kila rafiki unayealika kujiandikisha kwenye mtandao wa OpinionArena. Unapata alama mara moja baada ya rafiki kujiandikisha na kushiriki katika tafiti mbili.

Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kuwaalika marafiki

Jaza maelezo kujihusu

Pata pointi za ziada kwa kuongeza maelezo mafupi kujihusu. Maelezo zaidi unayoshiriki nasi, pointi zaidi utakazojipatia. Kuongezea, tutaweza kukutumia mwaliko kwenye tafiti zinazofaa zaidi.

Toa jibu kwa Uchaguzi wa haraka

Toa jibu kwa Uchaguzi wa haraka na upate pointi za ziada. Tunavutiwa na maoni yako kuhusu kila kitu: siasa, michezo, bei ya bidhaa, na kadhalika. Hebu tujue mwanasiasa maarufu, mwimbaji au mwanariadha, au gari maarufu zaidi! Kila wakati unapojibu, unapata pointi 3 za ziada kwenye akaunti yako.